CHEKI PICHA ZAO HAPA ZOTE...................SOMA HAPA.................NYUMA YAKE DIAMOND PLATINUMZ UNAJUA KUNA NANI? SOMA HAPA

0


  
HAKUNA ladha inayopendwa na mashabiki wa muziki Bongo kwa sasa kama Bongo Fleva. Zipo nyimbo nyingi ambazo zinapita masikioni mwa mashabiki na kufurahia lakini kizuri zaidi ni jinsi video za Bongo Fleva ambazo zimekuwa zikija kimataifa kila siku.

Wasafi Classic wakiwa katika pozi la pamoja ndani ya studio za Global TV Online.
Unapotaja kati ya video za muziki huo ambazo zipo juu kwa sasa ni wazi utataja moja kwa moja video za staa wa nyimbo hizo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kama vile Mdogomdogo, Nitampata Wapi, My Number One ambazo zote amezifanyia nchini Afrika Kusini.
Achana na video, twende kwenye shoo zake, Diamond ametokea kuteka majukwaa mbalimbali kwa kujaza nyomi ya watu. Miongoni mwa shoo zilizofanya poa ni pamoja na shoo za funga na fungua mwaka ambazo ni Usiku wa Wafalme iliyofanyika katika Ukumbi wa Dar Live, Mbagala-Zakhem, jijini Dar pamoja na ile iliyofanyika Uwanja wa Amahoro, Kigali, Rwanda.

Wasafi Classic wakiwa ndani ya ofisi za Global Publishers.
Je, Nyuma yake unajua kuna nani?
WCB kwa kirefu unaweza kuwaita Wasafi Classic Baby.
Kruu nzima ya WCB bado inaendelea kumfanya Diamond awe bora zaidi kwenye kila video hadi shoo. Katikati ya wiki hii, WCB ikiongozwa na meneja wao, Babu Tale walitinga katika mjengo wa Global Publishers uliopo Bamaga, Mwenge ambapo walifunguka mengi mbele ya waandishi wa mjengoni hapo.

Kwanza kabisa kuna Rais wa Wasafi, Diamond, chini yake kuna mameneja watatu wanaomuongoza ambao ni Babu Tale, Said Fella na Salam.Diamond hawezi kuamua mwenyewe avae nini aende wapi au afanye nini, kuna Q-Boy Msafi na Morgan ambao wapo kwa ajili hiyo. Baada ya hapo kuna msemaji wa kati ambaye pia ni DJ kwenye shoo zote tunazokwenda, Romy Jones.
WCB pia inaundwa na madansa nane ambapo wanaume wapo sita na wasichana wawili. Baada ya madansa kuna baunsa anaitwa Mwarabu Platnumz na hayupo kwa ajili ya kumuangalia Diamond tu bali yupo kuwaangalia WCB kwa ujumla. Ukiachana na baunsa kuna wapiga picha watatu lakini ambao tunasafiri nao ni wawili tu.WCB jumla inaundwa na watu 16.