CHEKI PICHA KIBAO NA STORI NZIMA YA HUYU JAMAA..........H.......UYU NDIYE ALIYEMPA ZARI JEURI YA FEDHA

0



Kibosile Ivan Ssemwanga akiwa na ‘Zari’.

Umaarufu wa msanii wa muziki, mjasiriamali na mkali wa fasheni kutoka Uganda anayeishi Afrika Kusini, Zarinah Hassan ‘Zari’ unazidi kupaa kila kukicha, habari ya mjini kwa sasa ikiwa ni malavidavi ya nguvu anayopeana na Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platinumz’.
Mfanyabiashara mkubwa wa Kiganda mwenye makazi yake nchini Afrika Kusini, Ivan Ssemwanga akipozi.

Wengi wanamjua Zari kutokana na urembo wa kipekee aliojaliwa na mkwanja wa kufa mtu, akiwa anamiliki ndinga za bei mbaya zikiwemo Ranger Rover Sports 2014, BMW, Black Chrysler, Audi Q7, Silver Crysler 2008, Mercedes Benz Convertible na nyingine kibao, zote zikiwa na ‘plate number’ inayosomeka jina lake la Zari.
Hata hivyo, ni wachache wanaojua siri ya utajiri wa mwanadada huyo ambaye kiasili baba yake ana mchanganyiko wa Burundi na Somalia wakati mama yake ana mchanganyiko wa Mhindi na Mganda.

IVAN SSEMWANGA NDIYO KILA KITU
Kabla ya kuanza ‘projekti’ na Diamond, Zari alikuwa ameolewa na mfanyabiashara mkubwa wa Kiganda mwenye makazi yake nchini Afrika Kusini, Ivan Ssemwanga ambaye anatajwa kuwa miongoni mwa mabilionea wachache kutoka Uganda, akiwa anaingiza faida ya zaidi ya shilingi za Uganda milioni 700 kwa mwezi (zaidi ya shilingi milioni 428 za Kibongo).

MALI ANAZOMILIKI IVAN
Achana na magari ya kifahari ambayo hayana idadi, yote yakiwa na ‘plate number’ yenye jina la Ivan, mchizi pia anamiliki Private Jet (ndege binafsi). Pia anamiliki utitiri wa vyuo vya Brooklyn City College, vikiwa na jumla ya ‘campus’ sita nchini Afrika Kusini katika Majiji ya Durban, Pretoria na Johannesburg, kila moja ikiwa na wanachuo kati ya 800 hadi 2100.

Watoto wa Zarinah Hassan, ‘Zari’.

Kozi zinazofundishwa kwenye vyuo vyake ni Information Technology (IT), Mining (uchimbaji wa madini) na Policing (Sera za biashara) ambazo zinapendwa na wengi Afrika Kusini, hali inayofanya apate wanachuo kibao.

Pia jamaa anamiliki bonge moja la mjengo lililopo Sir Apollo Kaggwa Road, Kampala pamoja na nyumba nyingine za kifahari zilizotapakaa maeneo ya Munyonyo, Bunga, Mutungo na Mukono nchini Uganda.

Pia jamaa anamiliki nyumba nyingine iliyopo Waterkloof Glen jijini Pretoria, Afrika Kusini na kuwa miongoni mwa Waganda wachache wanaomiliki nyumba nchini humo. Pia ana utitiri wa supermarkets, maduka ya vito vya thamani na maduka ya nguo (boutique) nchini Afrika Kusini.

KUFURU YA FEDHA
Hivi karibuni, Timu ya Taifa ya Uganda, Uganda Cranes ilikuwa na mechi dhidi ya Timu ya Taifa ya Zambia (Chipolopolo) ambapo jamaa alifanya kufuru ya aina yake kwa kutoa shilingi milioni 10 za Uganda (zaidi ya shilingi milioni 6 za Kibongo) kwa kila mchezaji na kuahidi kutoa shilingi milioni 5 za Uganda (zaidi ya milioni 3) kwa kila atakayefunga bao.

Zarinah Hassan ‘Zari’, 'The Boss Lady' akipozi.

Kama hiyo haitoshi, jamaa alikodi helikopta iliyombeba yeye na wapambe wake 10 aliosafiri nao kutoka Afrika Kusini na kuwalipia kila kitu kuelekea kwenye Mji wa Namboole, Uganda kushuhudia mechi hiyo ambayo hata hivyo Uganda haikushinda.

AMETOKEA WAPI?
Ivan aliyezaliwa kwenye familia yenye uwezo wa kawaida, alisafiri kwenda Afrika Kusini akitokea Uganda mwaka 2002 kwa msaada wa mpwa wake, Kyeyune aliyekuwa akifanya biashara ya magari ya kifahari Bondeni.

Baada ya kukaa naye kwa kipindi kifupi, Ivan naye alianza kujishughulisha na biashara hiyo ambapo alifanikiwa kutusua kinoma. Maisha yake yakabadilika, akaanza kuwekeza kwenye biashara nyingine nyingi mpaka akawa bilionea. Vijana wengi wa Afrika Kusini wanamtambua kwa jina la Shaba Wa Shaba 9 kutokana na uwezo wake wa kifedha.

ANAMPAJE JEURI YA FEDHA?
Rekodi zinaonesha kwamba kabla Zari hajakutana na bilionea huyo, alikuwa mtu wa kawaida sana, akijishughulisha na mambo ya urembo na saluni za kike lakini walipokutana, kupendana kisha kuoana, ndipo mwanadada huyo alipoanza kushaini kwa kuendesha ndinga kali na hadhi ya maisha yake ikabadilika.

Pia inaelezwa kuwa hata baada ya uhusiano wao kwenda mrama, bado Ivan anaendelea kumhudumia Zari na watoto wake watatu waliozaa pamoja, Pinto, Didy na Quincy kwa kuwapa mkwanja mrefu mara kwa mara huku mwanamke huyo akisimamia miradi mingi ya mwanaume huyo ambaye inaelezwa kuwa licha ya kutengana, hawajapeana talaka.

Huyo ndiyo Ivan Ssemwanga, kidume anayempa jeuri ya fedha Zari

PICHA ZOTE NA STORI NZIMA HII HAPA.........CHEKI BALAAAA LA DIAMOND HUKO NIGERIA LILIVYOKUWA.............P-SQUARE WAKUBALI UWEZO WA DIAMOND

0




MWACHENI Diamond aitwe Diamond! Hiyo kauli pekee unayoweza kuisema kufuatia wakali wa muziki wa R&B kutoka Nigeria, Peter na Paul Okoye ‘P-Square’ kuukubali uwezo wa kimuziki wa bwa’mdogo kutoka Tandale, Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
NI LAGOS, NIGERIA
Wakali hao walionesha kumpigia saluti Diamond baada ya kukutana naye kwenye tamasha la utoaji wa Tuzo za Wanamichezo Bora Afrika lililofanyika Lagos, Nigeria, usiku wa kuamkia Januari 9, mwaka huu.

  
Bwa’mdogo kutoka Tandale, Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa madansa wake ndani ya Lagos, Nigeria.

WALIANZIA HOTELINI
Kwa mujibu wa chanzo kilichoambatana na Diamond nchini humo, saa chache kabla ya shoo kuanza, P-Square walimuibukia kwenye Hoteli ya Eko aliyofikia jijini humo na kummwagia pongezi nyingi sambamba na kumshauri baadhi ya vitu vya kimaendeleo.

‘Diamond Platnumz’ akifurahia jambo na Peter Okoye wa 'P Square'.

TUJIUNGE NA CHANZO
Chanzo hicho kilisema, P-Square walionekana kuvutiwa zaidi na juhudi binafsi za Diamond kiasi cha kuweza kuipeperusha bendera ya Afrika Mashariki katika levo za kimataifa.
“Jamaa walipomuona tu hotelini waliguswa sana na juhudi zake binafsi maana wanatambua jinsi gani muziki ulivyokuwa mgumu kuuvusha nje ya nchi yako lakini kwa kuwa Diamond ameweza, walimpigia saluti,” kilisema chanzo hicho.

ARUHUSIWA KOLABO
Chanzo hicho kilizidi kumwaga data za ndani kwa kusema, mbali na kumpigia saluti, P-Square walionesha wako tayari kumsapoti Diamond kwa kumpa nafasi ya kufanya nao kazi yaani kolabo.
“Wamempa nafasi ya kufanya naye kazi pale atakapojisikia kutokana na mipango yake, kama akiamua kufanya sasa au baadaye ni uamuzi wake lakini jamaa (P-Square) hawana kinyongo naye lengo lao ni kuona muziki wa Afrika unateka dunia,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:
‘Diamond Platnumz’ akiwa na Paul Okoye wa 'P Square'.

“Walimwambia the way (namna) alivyo na juhudi kwenye kazi yake anatambulika Nigeria utafikiri ni msanii kutoka Nigeria, walimpa mbinu zao za namna walivyopigana hadi kufika hapo walipo.”

MASTAA WAMUIBUKIA
Mbali na P-Square, mastaa mbalimbali wa Nigeria walimuibukia Diamond hotelini hapo akiwemo Mr Flavour na Jude Abaga ‘M.I’, ambao walimpa pongezi Diamond kwa kujua kumiliki vyema jukwaa kwani wamekuwa wakifuatilia shoo zake hasa anapotupia video zake mitandaoni.

Msanii wa muziki kutoka Nigeria, Mr Flavour akiteta jambo na 'Diamond Platnumz'.

APIGA SHOO YA MAANA
Ulipofika wakati wa kupanda jukwaani, Diamond aliitikisa Nigeria kwani alionesha vitu vya tofauti wakati akiimba nyimbo zake na kuwafanya Wanigeria na waalikwa mbalimbali wapigwe na butwaa huku wengi wakiishia kumpigia makofi na shangwe la kufa mtu.

DIAMOND ANASEMAJE?
Paparazi alimcheki Diamond kupitia mtandao wa WhatsApp ambapo aliwashukuru mastaa hao wa Nigeria kwa upendo wao na kuahidi kuendelea kufanya maajabu zaidi katika levo za kimataifa.
“Wana wamenisapraizi hotelini, tumepiga stori nyingi, wameonesha wanakubali kile ambacho mimi nafanya, jukwaani nimefanya vizuri, watu na heshima zao mwishoni walipiga makofi kuonesha wamekubali.

KUHUSU KOLABO?
“Kuhusu kolabo na P-Square, ni mapema sana kuzungumzia kwa kuwa nina mipango mingi ya kufanya mwaka huu, mashabiki wakae mkao wa kula, nikiona inafaa, nitafanya nao maana wao hawana shida na mimi,” alisema Diamond.

P-SQUARE NI ZAIDI YA DAVIDO
Awali, kabla Diamond hajakutana na P-Square, alishirikiana na mkali mwingine wa Nigeria, Davido katika wimbo wake wa Number One Remix ambaye inaaminika kwa umaarufu na uwezo wa kimuziki yupo chini ya P-Square.

video: Kama kifaa chako kinauwezo bofya play hapa chini

BALAAAAAA LINGINE KWA WOLPER HATIMAYE AKUBALI KUPOSWA NA MANAIKI AMBAYE NI STAR WA PICHA ZA UTUPU

0


BAADA ya msanii wa filamu hapa Bongo, Manaiki Sanga kutangaza nia ya kutaka kumposa mwigizaji Jacqueline Wolper, staa huyo ameibuka na kumjibu kuwa na yeye yupo tayari kama ataweza kutimiza masharti.

Mwigizaji wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper akipozi na Manaiki.
Akizungumza na paparazi, Wolper alisema katika mila za Kiafrika, posa haikataliwi, inatolewa na kisha inajadiliwa kwa hiyo kama Manaiki kajipanga, apeleke posa ikajadiliwe na wazee wake.
“Nimesikia habari za Manaiki kutaka kuniposa nikacheka sana kwa sababu yeye kama yupo tayari apeleke posa itapokelewa kwani siku zote vigezo na masharti huzingatiwa, afuate utaratibu tu,” alisema Wolper.

PICHA ZOTE ZA TUKIO ZIMA ILIVYO KUWA HAPA.......................................RONALDO MWANASOKA BORA WA DUNIA 2014

0

 Cristiano Ronaldo has been crowned with the 2014 Ballon d'Or award after a stellar 12 months

MCHEZAJI wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ureno CRISTIANO RONALDO ametangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya FIFA ya Mwanasoka Bora wa mwaka 2014 maarufu kama FIFA BALLON D'OR ikiwa ni kwa mara ya pili mfululizo.
Ronaldo amewashinda Lionel Messi wa Barcelona na timu ya Taifa ya Argentina pamoja na golikipa wa timu ya taifa ya Ujerumani na bayern Munich manuel Neuer.
Ronaldo ameshinda kwa kupata 37.66% ya kura zote zilizopigwa, akifuatiwa na Lionel Messi aliyepata 15.76% wakati @Manuel_Neuer akipata 15.72% ya kura zote.
Katika Tuzo hizo, kocha wa timu ya Taifa ya Ujerumani Joachim Low ametajwa kuwa Kocha bora wa FIFA wa mwaka 2014, na James Rodrigues amepata tuzo ya bao bora la FIFA la mwaka 2014 na kutunukiwa tuzo ya FIFA PUSKAS AWARD kwa bao aliloifungia Colombia katika mchezo wa Kombe la Dunia dhidi ya Uruguay.

Kikosi bora cha FIFA ni Neuer; Lahm, Ramos, David Luiz, Thiago Silva; Di Maria, Iniesta, Kroos; Messi, Ronaldo, Roben
 Ronaldo was looking to win the Ballon d'Or award for a second successive year and the third-time in his career
 Ronaldo (left) enjoys a selfie with Marta before the FIFA Ballon d'Or Gala on Monday evening
The 29-year-old played an integral role as Real Madrid won the Champions League last season
 

Popular Posts

ONLINE VIEWS

Jicholamwewe.com.